Na Yusuph Mwamba
BAADA ya Tetemeko la ardhi kutokea nchini Italia na kuacha maafa makubwa, hali imekuwa sio shwari baada ya Maelfu ya watu katikati mwa Italia kulala katika magari na mahema ikiwa ni kama makazi ya muda mfupi baada ya tetemeko kubwa kupiga katika eneo hilo tokea kile cha mwezi Agosti.
Wakaazi katika eneo lililoathirika zaidi la Norcia wamesema walikuwa na hofu sana kuendelea kukaa ndani mwa nyumba zao.
![]() |
Baadhi ya wakazi walioathirika na tetemeko hilo wakiwa kwenye makazi ya muda |
Takriban watu 20 wamejeruhiwa na tetemeko hilo lililotokea siku ya Jumapili, lakini inasemekana mtu mmoja amepoteza maisha.
Mkuu wa eneo hilo Luca Ceriscioli amesema zaidi ya watu laki moja watahitaji msaada.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment