Halloween party ideas 2015
Image




Na Yusuph Mwamba
MAAFISA  nchini Saud Arabia,  wametekeleza adhabu ya kifo kwa raia mmoja wa Ethiopia aliyekuwa akifanya kazi za ndani baada ya kushtakiwa na kukutwa na hatia ya kumuua mtoto wa muajiri wake
Hayo yamezungumzwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia ambapo imesema  kuwa adhabu hiyo ya kifo imetekelezwa baada ya kuidhinishwa na mfalme wa nchi hiyo.
Mtuhumiwa alikiri kumuua kwa kumchoma kisu mtoto wa kike wa miaka sita mnamo mwezi Juni mwaka 2013 kwa madai ya kulipiza kisasi uonevu na mateso aliyokuwa akifanyiwa na familia ya mtoto huyo.
Kuuawa kwa kukatwa kichwa mtuhumiwa huyo kumeifanya idadi ya waliouawa chini ya adhabu ya kifo nchini Saudi Arabia kuwa watu 119 kwa ujumla mwaka huu, kwa mujibu wa shirika la habari la DPA.
Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu,  Saudi Arabia ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa utekelezaji wa adhabu ya kifo duniani.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.