Halloween party ideas 2015
Image

Ranieri1
Na Athumani Adam
“Can we?” “Yes we can”. Ni sentensi mbili fupi za lugha ya kingereza ambazo mgombea wa urais nchini Marekani, Barrack Obama alitumia sana wakati ule wa kampeni mwaka 2008. Yawezekana lengo la Obama kutumia sentensi zile alikuwa hajiamini kama anaweza kuwa raisi wa Marekani mwenye asilii ya bara la Afrika.
Hivyo mara zote aliwauliza wafuasi wake, can we? ‘yaani tutaweza?’, wafuasi wakimpa moyo ndio tutaweza yaani ‘yes we can’. Japokuwa ilikuwa ngumu kuamini lakini Obama alifanikiwa kuwa rais wa Marekani kupitia chama cha Democratic.
Mapema mwanzoni mwa msimu wa ligi kuu ya England, msimu huu mwaka 2015/16 unaanza hakuna aliyedhani kwamba klabu ya Leicester City ingeweza kuwa bingwa wa ligi, EPL. Hata kama endapo kocha wa timu hii, Mtaliano Claudio Ranieri angewauliza wachezaji wake kauli ya Obama kuhusu ubingwa, sidhani kama wangeweza kumjibu, lakini imetokea chini ya Ranieri baada ya miaka 132 tangu kuanzishwa klabu hiyo.
Ranieri ameingia kwenye vitabu vya historia vya Leicester, bila shaka atakumbukwa vizazi na vizazi vijavyo. Ranieri ni nani? Ametoka wapi? Makala hii inakupa majibu ya maswali ambayo ulikuwa unajiuliza kuhusu Mtaliano huyu.
  1. Claudio Ranieri ni nani?
Ni miongoni mwa makocha wa siku nyingi barani Ulaya. Alizaliwa mnamo tarehe 20/10/1951 kwenye mji wa Rome nchini Italia. Alianza rasmi kufundisha mpira mwaka 1987 baada ya kustaafu kucheza kwenye vilabu vya Catanzaro (1974-1982), Catania (1982-1984) na Palermo (1984-1986). Ranieri alikuwa anacheza nafasi za ulinzi
  1. Kwanini anaitwa Tinker Man?
Tinker ni neno la Kiingereza lenye maana ya kubadilika. Jina hili alipewa na Waingereza msimu wa 2002/03 alipokuwa na Chelsea. Ranieri alipewa jina hilo kwa sababu ya kubadili na kutumia wachezaji tofauti tofauti kwenye kikosi yaani ‘Rotation’
  1. Ranieri amewahi kufundisha timu zipi?
Leicester City ni klabu ya 11 kunolewa na Ranieri. Vilabu vingine ambayo zimewahi kuwa chini ya Mtaliano huyu ni Cagliari (1987), Napoli (1987-1989), Fiorentina (1993), Valencia (1997-1999  na 2004) Atletico Madrid, Chelsea (2000-2004), Parma (2007), Juventus (2007), Roma (2009), Inter Milan (2011) na Monaco (2012).
Mbali na kufundisha timu za vilabu, pia amewahi kufundisha timu ya taifa ya Ugiriki, baada ya Kombe la Dunia mwaka 2014.
  1. Ranieri amewahi kushinda Vikombe gani?
Ranieri amewahi kutwaa mataji mbali mbali barani Ulaya kwenye timu ambazo amezifundisha. Coppa Italia na Super Copa Italia (1996)-Fiorentina, Copa Del Rey (1999), UEFA Super Cup (2004)-Valencia, France Legue 2 (2012)-Monaco.
Ukiondoa mataji hayo, pia amewahi amefika fainali ya kombe la FA akiwa na Chelsea mwaka 2003 lakini alipoteza kwa Arsenal. Pia mwaka huo 2003 alicheza nusu fainali ya UEFA Champions League na kupoteza lakini alitolewa na Monaco
Mwaka 2007 alipoteza fainali ya kombe la Supercoppa Italia mbele ya Inter Milan. Mwaka 1987 alipandisha timu ya Cagliari kutoka Serie C hadi Serie A
  1. Ranieri amewahi kuwaamini wachezaji vijana?
Kama ilivyo kwa makocha wengine, Claudio Ranieri amewahi kuwapa nafasi vijana kwenye timu mbali mbali. Akiwa Napoli ya Italia alimpa nafasi mshambuliaji Gianfranco Zola kuchukua nafasi ya mkongwe Diego Maradona. Vile vile aliwapa nafasi Gaizka Mendieta, Miguel Angel Angulo na Javier Farinos wakati anafundisha Valencia ya Hispania
Kwenye dirisha la usajili mwaka 2001, alimnunua Frank Lampard kutoka Westham na kumpeleka Chelsea. Pia aliwapa nafasi wachezaji vijana John Terry na Robert Huth kwenye kikosi cha kwanza
  1. Amewahi kuwa na vita ya maneno?
Alipokuwa na Parma ya nchini Italia, ilitokea vita ya maneno baina yake Ranieri na aliyekuwa kocha mkuu wa Intermilan wakati huo mreno, Jose Mourinho
  1. Vipi kuhusu kufukuzwa kazi?
Kuna msemo maarufu makocha ‘huajiriwa ili wafukuze’. Ranieri amewahi kufukuzwa kwenye timu mbali mbali sababu ikiwa matokeo mabaya. Alitimuliwa kufundisha timu ya taifa ya Ugiriki baada ya kupoteza mechi ya kufuzu mataifa Ulaya Euro 2016 dhidi ya Visiwa vya Faroe
Alipokuwa Chelsea alifukuzwa baada ya kuiacha timu nafasi ya 6 kwenye ligi licha ya kupewa dau la usajili Euro milioni 120 na tajiri Roman Abromovich. Pia aliondolewa Atletico Madrid na Rais Jesus Gil sababu ikiwa ni matokeo mabaya.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.