Kesi dhidi ya mwanamke mfanyabiashara raia wa
China anayetuhumiwa na mashtaka ya kuendeleza mtandaoa wa kihalifu wa ulanguzi
wa pembe barani Asia imeahirishwa kwa wiki mbili nchini Tanzania.
Alifikishwa mahakamani Jumatatu
asubuhi mjini Dar es Salaam.
Waendesha mashtaka wanasema Yang
Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa pembe, aliendesha
biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao
ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia.
Anashutumiwa kwa kuendeleza
shughuli hiyo kwa takriban miaka 14.
Anakana mashtaka hayo.
Mahakama imeambiwa kwamba faili
ya kesi yake bado imo mikononi mwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma.
Maafisa wa serikali Tanzania
walitaja kukamatwa kwa Yang Feng Glan mnamo Oktoba mwaka jana kama
Taifa hilo la Afrika mashariki
limepoteza thuluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka miwili
Post a Comment