AUA MKE NA MTOTO
Mama mmoja na mtoto wake wameuwawa huko kaole bagamoyo kwa kuchinjwa shingoni kwa kisu na mme wake kwa kilichosemekana
kuwa ni wivu wa mapenzi.
Tukio hilo lilitokea jana saa kumi jioni wakati mama huyo aliyetambulika kwa jina la Oliver Erasto mkazi wa Kawe(22) na mwanae Emanuel Flowin`walipokuwa wameenda kutembelea nyumba yao inayondelea kujengwa huko Kaole Bagamoyo.
Peter Mbwale (26) mkazi wa Kawe ambae ni baba wa familia alitumia mbinu hiyo ya kumdanganya mke wake kuwa wanaenda kuangalia nyumba yao inayoendelea kujengwa huko Kaole Bagamoyo ili akamilishe lengo lake la kumchinja mke wake akishirikiana na rafiki yake Rajabu Juma(20) mkazi wa Makongo jijini Dar es Salaam.
Miili ya marehemu ilikutwa umbali wa mita 100 kutoka barabara na washitakiwa wote wawili wamekiri wazi kufanya tukio hilo.
Post a Comment