Halloween party ideas 2015
Image

Waombolezaji kote Thailand wanafanya matembezi kunaadhimisha sehemu kuu ya siku tano za sherehe za mazishi kwa ajili the Mfalme Bhumibol Adulyadej aliyeaga dunia.
Mfalme wa Thailand Bhumibol Adulyadej
Mfalme huyo alifariki Oktoba 2016 akiwa na umri wa miaka 88.
Mwili wake utateketezwa kwa moto baadaye Alhamisi, Kwa taratibu za kifalme zitakazoongozwa na mwanae na mrithi wake, Mfalme Maha Vajiralongkorn.
Taratibu za mazishi zilianza Jumatano kwa sherehe za kubudha ,kwenye kasri Kuu la kifalme.
Waombolezaji
Leo Alhamisi imetangazwa kuwa siku ya mapumziko, ambapo biashara nyingi zitafungwa kwa siku ama kwa nusu siku.
Mapema Alhamisi, mwili wa mfalme huyo utaletwa kwenye eneo maalum utakapochomwa kutoka kwenye Ukumbi waKifalme ulipo katika Kasri kuu kwa ajili ya uteketezwa.
Wajumbe wa familia ya ufalme wa Thailand na waheshimiwa kutoka nchi 40 watahudhuria mazishi hayo ya kuchomwa kwa mwili wa hayati mfalme Bhumibol Adulyadej , huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kujipanga kwenye mitaa ya karibu.
Majivu ya Mfalme hatimae yatakusanywa na kusafirishwa hadi kwenye kasri la Ufalme Ijumaa.
Sherehe zitaendelea kwa siku mbili zaidi.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.