London , Uingereza
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Hispainia na klabu ya soka
ya Chelsea Diego Costa, amemtolea uvuvi kocha wake baada ya kukerwa na maamuzi yanayoendelea kufanyika klabu hapo dhidi yake.
Costa mwenye umri wa miaka 29, amesikitishwa na kitendo
cha Kocha wake kuonesha dhahiri ubaguzi dhidi
yake, hatua iliyompelekea kumshusha
thamani kocha huyo aliyekua akimuheshimu kipindi chote alichodumu na kutumikia kunako
klabu hyo.
Aidha, nyota huyo alisema kuwa, hawakua katika mahusiano
mazuri kipindi cha kuelekea mwisho wa ligi hiyo 2016/2017 licha ya yeye kuwa na
mchango mkubwa kuiwezesha Chelsea
kunyakua ubingwa wa ligi hiyo lakini alionekana sikitu mbele ya kocha huyo.
Wakati wa kujiandaa na usajili baada ya dirisha
kufunguliwa, Conte, alimtumia ujumbe wa maandishi nyota huyo na kumueleza
kwamba hayupo katika mipango yake ya usajili hivyo atafute timu nyingin jambo
lililompelekea Mhispainia huyo kutaka kurejea kunako klabu yake ya zamani ya
Atletico Madrid.
Lakini katika mahaojiano na Daily Mail, Costa,
alielezea wa kina kuhusiana na mgogoro
uliokuwepo dhidi ya kocha huyo Mtaliano
pamoja na kuvunjika kwa uhusiano
ya wawili hao.
Costa, ambaye ni mchezaji mtukutu uwanjani lakini
hakusita kuonyesha hisia zake na mapenzi yake Chelsea kwani lengo lake lilikuwa
baada ya kumalizika kwa makataba wake aongeze mwenigine jambo lililoonekana
kwenda kinyume na matakwa ya bosi wake ambaye hakutaka kuendelea nae katika
msimu mpya ulioanza hivi karibuni.
Kwa upande wa mwanansheria wa mwanandinga huyo, Ricardo
Cardoso, alisema kilichokuwepo sasa ni kutaka kufungua mashtaka dhidi ya klabu ya Chelsea kulazimisha kumuuza mteja
wake kwa klabu nyingine au kuzungumza na
nyota huyo ili waweze kufikia muafaka nasio kuendelea kumnyanyasa .
"Ninamheshimu kama kocha mkuu, amefanya kazi nzuri Chelsea hilo nimeliona lakini kasoro
iliyokuwepo ni kwamba hana utu wala hayupo karibu sana na wachezaji wake jambo
ambalo litapelkea kuwagawa wachezaji na kuruhusu upotevu wa nyota kutimka klabuni
hapo”, Alisema Ricardo
Msimamo wa Chelsea ni kwamba Costa na wawakilishi wake
walitambua kuwa wakati wake Stamford Bridge ulikuwa ukimalizika Januari, wakati
ilipokuja hoja ya mafunzo , lakini mshambuliaji huyo alithibitisha kwamba
mgogoro haukutoka kutokana na kuumia nyuma, kama ilivyoripotiwa hapo awali.
Licha ya malalamiko ya Costa, klabu ya Chelsea ilianza
utetezi wao wa kutetea kombe la ligi kuu Uingereza 2017/2018 kwa kuambulia
kichapo cha jumla ya mabao 3-2 dhidi ya Burnley kwenye uwanja Stamford Bridge
siku ya Jumamosi.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment