Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani
MENEJA  wa klabu ya soka ya  Manchester United, Jose Mourinho, anasema kuwa amefanya uamuzi kuhusu winga wa klabu ya Manchester United Adnan Januzaj lakini akakataa kusema uamuzi aliochukua.
Januzaj, ambaye ni raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 22, amehudumu msimu wote kwa mkopo katika timu ya ligi ya Uingereza Sunderland, ambapo itacheza na United siku ya Jumapili.
Ana kandarasi ya hadi 2018 katika klabu ya Manchester United.
''Nimeamua lakini sitamwambia mtu yeyote'', alisema Mourinho siku ya Ijumaa wakati alipoulizwa kuhusu hatma ya Januzaj.

Amefunga mabao 5 katika mechi 63 za United.

Januzaj alihudumia miezi minne katika mkopo katika klabu ya Bundesliga Borussia Dortmund msimu uliopita, lakini alicheza mechi 12 pekee kabla ya kurudi katika timu yake ya Manchester United.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.