Na Mwanaidi Mziray
KISWAHILI ni lugha ya taifa ya Tanzania,lakini lugha hii kwa sasa inazidi kukua na kuzungumzwa nje ya nchi kama vile Kenya na Uganda na nchi nyingine nyingi, lakini lugha yeyote ili haiwezi kukua bila kuipenda na kuitumia lugha husika.
Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katika mazingira ya vituo vya biashara vya pwani ambakowafanyabiashara kutoka Uarabuni, Uajemi na Uhindi walikutana na wenyeji Waafrika. Lugha kuu ya kimataifa ya biashara hiyo ilikuwa Kiarabu.
Inaonekana ya kwamba lugha mpya ilijitokeza wakati wenyeji wa pwani, waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu, walipopokea maneno mengi hasa ya Kiarabu katika mawasiliano yao. Kwa hiyo msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. Imekadiriwa ya kwamba karibu theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.
Kuanzia karne ya 20 hadi sasa maneno mengi yamepokewa kutoka Kiingereza, na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kifaransa, lakini pia kutoka lugha nyingine, Kiarabu kikiwa mojawapo.
Kwa karne nyingi iliandikwa kwa herufi za Kiarabu (سواحلي sawaHili au لغة سواحيلية lugha sawaHiliya).
Sarufi ya kwanza pamoja na kamusi iliandikwa mwaka 1848 na Dr. Ludwig Krapf huko Rabai Mpya /Mombasa.
Kiswahili kilikuwa na lahaja nyingi kutokana na lugha mbalimbali za Kibantu zilizochangia katika eneo husika.
Tangu karne ya 19 lugha ilianza kuenea barani kwa njia ya biashara.
Wakati wa ukoloni wa Uingereza lugha ilisanifishwa na Kamati ya kimaeneo ya lugha ya Kiswahili kwenye msingi wa lahaja ya Unguja.
Kiswahili kimekuwa lugha rasmi katika nchi zifuatazo:
- Tanzania: ni lugha ya taifa; ni lugha ya shule za msingi, lugha ya utawala serikalini na mahakamani; inatumika kote nchini, makanisani, misikitini, redioni, kwenye runinga na idadi kubwa ya magazeti. Serikali inatakiwa kukiendeleza Kiswahili kwa sababu ni lugha ya taifa. Sera ya elimu ya mwaka 2015 imechagua Kiswahili katika miaka 10 ijayo kiwe lugha ya kufundishia katika ngazi zote, ikiwemo ile ya chuo kikuu
- Kenya: ni lugha ya taifa lakini Kiingereza ni lugha rasmi ya kiutawala; Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wananchi wakikutana nje ya eneo lenye kabila moja tu; ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni; ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wananchi mjini na kitaifa; sehemu za ibada makanisani zinatumia Kiswahili; kuna gazeti moja tu la Kiswahili; sehemu za programu redioni na kwenye runinga ni kwa Kiswahili. Lugha inachanganywa mara nyingi na Kiingereza na lugha za maeneo au za kikabila. Hata hivyo baada ya rasimu ya katiba mpya kupitishwa tarehe 4 Agosti 2010, Kiswahili sasa kitakuwa lugha rasmi, sawa na Kiingereza.
- Uganda: kimetangazwa kuwa lugha ya kitaifa tangu 2005; iliwahi kuwa lugha ya kitaifa wakati wa utawala wa Idi Amin; wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango hiyo. Ni lugha ya polisi na jeshi, hali ambayo imeleta ugumu kwa lugha kukubalika na wananchi wengi kutokana na historia ya utawala wa kijeshi Uganda; watu wengi bado hukumbuka hasa matusi ya wanajeshi waliowatesa wakisema Kiswahili. Lakini kuna maeneo ya Uganda ambako Kiswahili kinatumiwa na watu wengi kama lugha ya sokoni na barabarani. Wona UBC, WBS tv.
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Kiswahili ni kati ya lugha nne za kitaifa, pia lugha ya jeshi katika mashariki ya nchi. Kiswahili kimefika na misafara ya biashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani ya Tanganyika. Imeenea zaidi kati ya mchanganyiko wa wafanyakazi kwenye migodi ya Shaba.
Lugha ya kwanza, lugha ya pili
Kiasili Kiswahili kilikuwa lugha ya kwanza tu ya wakazi wa miji ya Waswahili kwenye pwani, katika sehemu za pwani pia kijijini. Baada ya kuenea kimekuwa lugha ya watu wengi mjini hasa Tanzania lakini pia Kenya.Kimeenea zaidi kama lugha ya mawasiliano na biashara pale ambako watu wa makabila mbalimbali wanakutana. Pamoja na nchi zinazotajwa hapo juu Kiswahili kinatumika katika Kaskazini ya Msumbiji, Kusini kabisa ya Somalia, Mashariki ya Burundi.Tanzania na Kenya zilipokea wakimbizi wengi waliojifunza Kiswahili lakini hakuna uhakika kama bado kinatumika wakirudi Rwanda, Sudan au Somalia.Kimataifa
Lugha hii leo imekuwa na umuhimu mkubwa duniani kwa jumla, na hasa Africa, kwa sababu ya kuenea kwake nchi mbali mbali, na kukusanya kwake watu wa makabila na nchi kadha wa kadha wakaweza kufahamiana kwa lugha moja, hasa ilivyokuwa ni lugha mojawapo katika lugha kubwa za Africa ambazo zinachukuwa mahala pa lugha za kigeni na Wakoloni, kama Kiarabu, Kiurdu, Kiebrania, Kireno na kadhalika.Leo, imekuwa inatumiwa katika kusambaza habari katika vituo mbali mbali ulimwenguni kama vile Sauti ya Amerika, BBC, Deutsche Welle, Monte Carlo, na nchi nyinginezo za Uchina, Urusi, Irani na kwengineko.Aidha, imekuwa ni mojawapo ya lugha muhimu zinazofundishwa katika vyuo vikuu nchini Marekani, Uingereza, Ulaya bara, Urusi, Uchina, na barani Afrika.Maendeleo ya Kiswahili
Lugha ina maendeleo: inaweza kukua, kukwama au kufa. Athira nyingi hutokea bila mpangilio pale ambako wasemaji wanapokea maneno mapya, wanaacha kutumia maneno mengine au hubadilisha kawaida ya matamshi au sarufi. Haya yote hutokea pia katika uwanja wa Kiswahili.Kuna mzaha unaosimuliwa hasa Tanzania: Kiswahili kilizaliwa Unguja, kilikua Tanzania Bara, kikafa Kenya na kuzikwa Uganda. Hali halisi Kiswahili kina maendeleo yake katika nchi hizo zote labda zaidi Kongo.Lakini itategemea pia juhudi za serikali kama umoja wa lugha utatunzwa kwa sababu kuna athari nyingi kutoka lugha za kila eneo zinazoingia katika ukuzi wa Kiswahili kwa namna zinazotofauitiana.Taasisi zinazokuza Kiswahili
Kuna taasisi zinazolenga kukuza na kuimarisha Kiswahili kama vile Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vingine vya Kenya na pia Uganda.Nchini Tanzania kuna Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) ilhali nchini Kenya kuna Chama cha Kiswahili cha Taifa(CHAKITA). BAKITA na CHAKITA pamoja na wawakilishi kutoka Uganda wanaandaa kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki (BAKAMA).
Mwalimu Julius kambarage nyerere, alikuwa kipaumbele katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi kwa kuendesha shughuli zote za kijamii kama vile ,siasa,serikali na kiuchumi kwa lugha ya Kiswahili, mwaka 1962 baada ya uhuru mwl Julius Kambarage Nyerere, alihutubia bunge la kwanza kwa lugha ya Kiswahili ikionesha ni lugha yenyekupendeza kwa watanzania.
Aidha, mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliwafanya watanzania kuwa wamoja baada ya kufanikiwa katika jitiada zake za kuondoa ukabira ili kuweza kutumia lugha mojakatika kuleta maelewano na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii kwa kutumia lugha ya Kiswahili, lakini hamu iliyokuwepo mwanzoni ya kukuza lugha hii ya kiswahili kwa watanzania imetoweka ghafla.
Kwasasa, misamiati ya lugha ya Kiswahili inazidi kuongezeka kama vile neno MUBASHARA ni neno lenye asili ya kihindi lenyemaana ya moja kwa moja pamoja na misamiati mingine mingi hata hivyo vyombo vya habari pia vimekuwa msaada mkubwa katika kukuza na kueneza Kiswahili kwa njia mbalimbali kama vile kwa njia ya utangazaji pamoja na kuandika magazeti kwa lugha ya Kiswahili.
Hata hivyo, tasnia nzima ya uandishi wa habari hapa nchini, wakishirikiana na taasisi nyingine walijitoa kwa dhati katika kupambana katika kushirikiana vyema katika kutaarifu uma juu ya matumizi ya lugha ya Kiswahili, hii imedhihirishwa na Dk Ayubu Rioba, mkurugenzi shirika la utangazaji TBC.
Mbali na jitihada hizo za kukuza na kueneza lugha hii ya Kiswahili, pamekuwa na changamoto mbali mbali kwa watumiaji wa lugha husika kwa kuwa na kasumba yakwamba ukujua kingereza ndiyo unaonekana msomi hivyo pamekuwa na ongezeko kubwa la watanzania kuwa na uzalendo wa kujifunza lugha ya kigeni lugha ya kingereza ilihali lugha ya Kiswahili ni lugha ya taifa lakini watanzania wanaipiga teke asili yao.
Licha ya wazawa wengi kuwa na kasumba ya kujifunza lugha hiyo ya kigeni,imeonekana wageni kutoka mataifa mbalimbali kuwa na shauku ya kujifunza lugha ya Kiswahili kuliko wenyeji wa lugha hiyo,hii inaashilia dalili mbaya kwa watanzania kwani wanaweza kuididimiza na kuipoteza kabisa lugha hii ya Kiswahili.
"nimekuja Tanzaniakuendelea na shahada ya pili ya kujifunza lugha ya Kiswahili hivyo natarajia nitakapo rudi china naamini nitakuwa mwalimu wa Kiswahili,na lugha hii itakuwa kama daraja kati ya Tanzania na China hivyo nashangaa sana kuona watanzania kutokuipatia nafasi ya kipekee”.Alisema HON-CHUI raia wa china.
Katika upande wa sekta ya elimu lugha ya Kiswahili ina tumika kama lugha ya kufundishia katika ngazi ya ya elimu ya msingi na lugha ya kingereza inatumika kama somo,kuanzia ngazi ya sekondari na kuendelea lugha ya Kiswahili inatumika kama somo na masomo mengine lugha ya kingereza inatumika kama lugha ya kufundishia.
Hivyo tunaona lugha ya kingereza imepewa nafasi kubwa kuliko lugha ya taifa la Tanzania lugha ya Kiswahili katika ufundishaji ,je mwanafunzi ambae yupo shule ya msingi anatengenezewa mazingira gani atakapofika ngazi ya elimu ya sekondari? Na shule ya msingi amesoma kwa kutumia ligha ya Kiswahili na ndo anatarajia sekondari kusoma kwa lugha ya kiingereza.
Sasa kwa mtindo huu wa miundombinu ya elimu kama hivi panakuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi kufeli na pengine mwanafunzi anafeli kwa sababu ya kutokuelewa lugha.Dk Said Sima, mwalimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam, alitoa tathimini zake juu ya utofauti wa mwanafunzi anaesoma kwa lugha ya ambayo ni lahisi kuelewa na kuifanyia mtihani.
“Kiswahili hakizuii kingereza kutumika ila inaitajika kuzisimamia hizi lugha na katika utumiaji wa lugha ya Kiswahili katika kufundishia husaidia kwa asilimia kubwa kwa mwanafunzi kuelewa somo husika”Alisema Dk Sima
Aidha, Dk Sima, amemaliza kwa kutoa takwimu za tafiti ya mwaka2011 wa Jonson, kuwa mwanafunzi aliyesoma lugha ya kiingereza na kufanya mtihani kwa lugha hiyo ya kingereza ,mwanafunzi huyo atapunguza asilimia 20% ya uelewa.
“Lugha ya Kiswahili inabidi kipewe nafasi ndani na nje ya nchi katika nyanja mbalimbali lugha hii tuiangalie kama bidhaa hivyo inatupasa tusukume gurudumu la maendeleo ya Kiswahili tusipofanya hivyo tutabaki kuwa kama watazamaji,walalamikaji na wasindikizaji”Alisema mbunge wa bunge la afrika mashariki Shyrose Bhanji
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment