Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru yatakayofanyika Desemba 9 Mwaka huu katika Viwanja vya Uhuru Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya kuunga Mkono viongozi waliotangulia na waliopo kwa kuilinda na kuitunza amani ya nchi.

RC Makonda ameeleza kuwa ikiwa ni mara ya kwanza kwa maadhimisho hayo kufanyika tangu serikali ya awamu tano iingie madarakani, maadhimisho yatapambwa na kauli mbiu ya Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Kuimarisha Uchumi.


Aidha, RC Makonda amewataka watanzania kuibeba kauli mbiu hiyo na kupambana na rushwa na ufisadi kwa vitendo ili taifa liweze kusonga mbele na kuifikia hadhima ya Rais Magufuli kwenye Tanzania ya Viwanda ambayo itapatikana bila kuwepo kwa rushwa na ufisadi.

RC Makonda ameongeza kuwa Mgeni wa Heshima katika Maadhimisho hayo anataraji kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, ambaye atashuhudia shughuli mbalimbali katika viwanja hivyo na kulihutubia Taifa.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.