Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

TATIZO la hati limeonekana kuwa pana hususani kwa wale wenye umiliki, Kwa wale ambao tayari wana hati za majumba au viwanja wanajua wazi kuwa hati hizo zimeandikwa muda maalum, tofauti na wengi wanavyofikiria hasa wale ambao pengine hawajamiliki ardhi au wanamiliki ardhi lakini hawamiliki nyaraka hii.

Hati unayopewa ina muda maalum wa kuishi. Sio kweli kwamba ukishapata hati basi ndio umemaliza, hapana. Kama ilivyo kwa bidhaa nyingine au nyaraka nyingine kwa mfano leseni za kuendeshea vipando vya moto ambazo huisha muda (expire) ndivyo ilivyo kwa hati za nyumba/viwanja pia ambazo nazo huisha muda wake ( expire).

Waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh. William Lukuvi, amesema zaidi ya nyumba 35,000 zilizopo katika jiji la Mwanza hazina hati, jambo linalosababisha serikali kupoteza zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwaka kutokana na asilimia 88 ya nyumba kutolipiwa kodi katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo jijini Mwanza wakati wa uhamasishaji wa urasimishaji wa makazi holela, sambamba na utekelezaji wa mpango kabambe wa miaka 10 wa jiji la Mwanza utakaowawezesha wananchi kupanga, kupima na kumilikishwa ardhi na nyumba zao, huku akiagiza waliojenga maeneo hatarishi kujiandaa kuondoka kabla serikali haijawafikia kwani lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa kufikia juni 30 mwaka 2017 watu wote wawe wamepimiwa maeneo yao na kupewa hati.

Aidha, waziri Lukuvi amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watu wakiwemo maafisa ardhi kwenda mitaani kinyemela bila kupitia ofisi za serikali hasa nyakati za usiku kwa lengo la kuwaonyesha viwanja wananchi.

 Kiomoni Kibamba ni mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza, anasema zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa jiji la Mwanza wanaishi kwenye makazi holela, hatua ambayo imeilazimu wizara ya ardhi, nyumba na makazi kubuni mradi wa urasimishaji wa makazi holela, je nini matokeo ya utekelezaji wa mradi huo.

Waziri Lukuvi ametangaza rasmi kwamba kuanzia sasa michoro ya mipango miji itaanza kutolewa mwanza badala ya kupelekwa dar es salaam kwa mikoa mitano ya kanda ya ziwa, ambapo amteua deo kalimenzi ambaye ni afisa mipango miji wa jiji la mwanza kuwa mkurugenzi msaidizi wa mipango miji na vijiji wa kanda ya ziwa atakayehusika na kuidhinisha michoro ya mipango miji.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.