Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani

MAKAMU wa Rais aliyefutwa kazi nchini Sudan Kusini Riek Machar, ambaye aliikimbia nchi hiyo mwezi Agosti, ameapa kwamba atarejea nchini humo.

Amesema bado anapendwa na watu wa taifa hilo,AKiongea kutoka Afrika Kusini, Bw Machar ameambia BBC kwamba kundi lake la waasi bado lina matumaini ya kuingia kwenye mkataba wa amani na Rais Salva Kiir.

Amesema hayo licha ya mapigano makali kutokea mjini Malakal kati ya wanajeshi watiifu kwake na wanajeshi wa Rais Kiir.

Akiongea na kipindi cha HARDtalk cha BBC, Bw Machar amesema: "Nitarejea Sudan Kusini."
"Kwa sababu Rais Salva Kiir hataki uchaguzi huru na wa haki, ndio maana akatushambulia, alianzisha tena vita.
"Lakini natumai kwamba viongozi wenye busara na hekima kutoka kanda hiyo, na Afrika, na maeneo mengine ya dunia wataanzisha mchakato wa kisiasa ambao utarejesha tena amani, na kufufua mkataba wa amani na kuundwa tena kwa serikali ya mpito wa umoja wa kitaifa."
Bw Machar pia amekanusha madai kwamba alichochea vita na badala yake akasema wanajeshi wake walikuwa wanajilinda dhidi ya mashambulizi kutoka kwa wanajeshi wa serikali.

Machar, ambaye baada ya kutoroka Sudan Kusini alikimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na baadaye akaenda Khartoum, Sudan Kusini, kwa sasa anapokea matibabu Johannesburg.

Maafisa wa Rais Kiir wamewatuhumu wanajeshi wa Bw Machar kwa kuanzisha mashambulio hao.
Pande zote mbili zimetuhumiwa kwa kutekeleza uhalifu wakati wa vita.
Majuzi, shirika la Amnesty International lilipendekeza kuundwe mahakama maalum nchini humo ya kuchunguza waliotekeleza uhalifu wakati wa vita.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.