Serikali imesema
itahakikisha inaendelea kuwasimamia wakandarasi wa Ujenzi wa Barabara
kuhakikisha wanajenga barabara zote
nchini kwa viwango vilivyokusudiwa na
kumaliza kwa wakati ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa
wananchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa leo jijini Dar es salaam mara baada ya
kukagua Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano
jijini humo ambapo ameridhishwa na kasi
ya utekelezaji wake na kusisitiza kwa Wakala wa Baraba (TANROADS), mkoa wa Dar
es salaam kuwa wakali katika usimamizi ili kuhakikisha barabara hizo zinajengwa
kwa viwango vilivyokubaliwa kwenye mkataba.
“ Serikali imekuwa ikitumia Fedha nyingi katika
kutekeleza miradi hii, hivyo TANROADS hakikisheni mnasimamia wakandarasi hawa
kujenga barabara hizi kwa viwango na kwa wakati”, amesema Waziri Mbarawa.
Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa utekelezaji wa
awamu hiyo unaendelea vizuri ambapo
unahusisha barabara ya Kifuru – Msigani (km 4.5) ambayo kwa sasa imefika
asilimia 87, Goba – Makongo (km 4.5), nayo imefikia asilimia 52 na Goba –
Madale (km 5) yenye asilimia 5.
Profesa Mbarawa ametoa wito kwa wananchi wa maeneo
hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi naTANROADS mkoa wa Dar es salaam
wakati mradi huo ukiendeleaa kutekelezwa ili kusaidia kumaliza kwa wakati.
Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali inaendelea
kushughulikia suala la ulipaji wa fidia kwa wananchi wa maeneo hayo ambao
wamepitiwa na mradi huo.
Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es
salaam, Mhandisi Julius Ndyamkama, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa
watasimamia mradi huo usiku na mchana
ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyo bora.
Mhandisi Ndyamkama amebainisha changamoto
zinazowakabili katika utekelezaji wa mradi huo ikiwemo suala la ulipaji wa
fidia kwa baadhi ya maeneo hasa katika kipande cha barabara chenye urefu wa
kilometa 1 kuanzia Mto Mbezi kuelekea Makongo.
Naye, Mratibu wa Mradi wa barabara ya Goba – Madale
(km 5), kutoka kampuni ya Ujenzi ya Mwananchi Engineering and Contracting Co.
Ltd (MECCO), Mhandisi Crispin Mwombeki,
amesema kuwa tayari wameshakamilisha usanifu wa mradi na wanategemea kuanza
kazi za Ujenzi hivi karibuni.
Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya mradi wa Ujenzi wa
barabara za kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam umeanza
mwezi Desemba, mwaka 2016 ambapo umehusisha
barabara tatu za Kifuru – Msigani (km
4.5), Goba – Makongo (km 4.5), na Goba – Madale (km 5) na kugharimu Jumla ya
Shilingi Bilioni 24.2.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment