Halloween party ideas 2015
Image


Na Ahmed Makongo, Bunda


MTOTO mmoja ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katia shule ya msingi Bunda A, iliyoko wilayani hapa, katika mkoa wa Mara, Fransisco Issa, (11), mwenye picha hiyo hapo juu, amepotea katika mazingira ya kutatanisha wakati akiwa nyumbani kwao, kata ya Bunda Stoo mjini hapa..



Jeshi la polisi wilayani hapa limesema kuwa tayari taarifa ya kupotea kwa mtoto huyo imetolewa na wazazi wake kwa namba BND/RB/2374/2017.

Baba mzazi wa mtoto huyo Issa Majura alisema kuwa mtoto huyo alipotea mwezi wa tano mwaka huu, majira ya saa nne asubuhi, wakati wakiwa kwenye michezo ya umitashumta mjini hapa.

Alisema kuwa mtoto huyo alikuwa na tabia ya kuondoka nyumbani hapo mara kwa mara na kwamba siku moja aliondoka na kuletwa usiku na mlinzi mmoja wa kikundi cha  Sungusungu baada ya kumkuta katika maeneo hatarishi, ambayo siyo rasmi kwa watoto.

Mama mdogo wa mtoto huyo Nice Andrea alisema kuwa siku aliyopotea kabla ya kuondoka nyumbani hapo na kwenda kwenye michezo hiyo aliwaambia wenzake kuwa anaondoka nyumbani hapo na hatarudi tena.

“Alikuwa na tabia ya kuondokaondoka, lakini siku hiyo alisema anaondoka na harudi tena na kweli tangu siku hiyo hakurudi hadi leo. Tumekwisha mtafuta sana lakini bado hatujampata” alisema Nice.

Wazazi wa mtoto huyo wanawaomba wananchi popote watakapomuona mtoto huyo, wawasiliane nao kwa namba za simu zifuatazo, ya baba yake mzazi Issa Majura 0767770375 au ya mama yake mdogo ambayo ni 0759295961, au ya ndugu yake ambaye ni afisa kilimo katika wilaya ya Bunda, Blandina Mulemwa kwa namba za simu 0784401144 na 0652445215,

Aidha, wawasiliane na mwandishi wa habari hii, Ahmed Makongo, kwa namba za simu 0765647577/0784643040/0655643040, au watowe taarifsa kituo chochote cha polisi.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Attachments area

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.