Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
MANOWARI za Urusi, ambazo zilikuwa zimetarajiwa kusimama Uhispania kuongeza hazina ya mafuta, hazitasimama nchini humo tena kutokana na wasiwasi wa mataifa wanachama wa Nato.

Urusiinaripotiwa kuondoa ombi lake la kutaka meli hizo za kivita zitie nanga katika bandari ya Cueta.
Wizara ya mambo ya nje ya Uhispania amekiri kwamba meli hizo hazitasimama katika pwani yake.
Uhispania imekuwa ikishinikizwa na mataifa wanachama wa shirka la kujihami la nchi za Maghafibi, Nato, kutoruhusu meli hizo zinazoelekea Syria kuongezwa mafuta kwenye bandari zake.
Kundi la meli za kivita za Urusi zimekuwa zikielekea bahari ya Mediterranean kusaidia kutekeleza mashambulio dhidi ya waasi wanaopinga Rais Bashar Assad.


Urusi ilikuwa awali imepewa ruhusa ya kuingiza meli tatu bandari ya Cueta kati ya 28 Oktoba na 2 Novemba.

Nato imekua ikipinga  yanayotekelezwa na Urusi nchini Syria, na inahofia meli hizo zitatumiwa kuzidisha mashambulio dhidi ya maeneo yenye raia Aleppo.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.