Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

WAKATI Dunia ikelekea katika kujinasau na umasikini na kuhakikisha jamii inapiga hatua kwa Nyanja zote za kiuchumi, kijamii, utamaduni na elimu, bila shaka ujio wa maadhimisho hayo utaleta tija sana kwa nchi ambazo zipo katika ulimwengu wa tatu yaani Mataifa yanayoendelea.







SACCOS Madhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kila mwaka Siku ya Alhamisi ya tatu ya mwezi Oktoba, ambapo kwa mwaka huusiku hiyo itakuwa ni tarehe 13 Oktoba 2016.
Maadhimisho ya mwaka huu yanatarajia kiufanyika Jijini Dar es salaam, Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa takribani siku tatu za tarehe 11-13 Oktoba 2016, na imepangwa kuwa mbali na maonesho ya bidhaa na huduma zitolewazo na na wadau wake zilizopangwa kufanyika kwa siku zote tatu.
Siku ya kwanza imetengwa kama siku maalumu ya ufunguzi rasmi wa maadhimisho hayo, siku ya pili ni kwa ajili  ya Kongamano la wana Saccos na wadau Wakuu wa SACCOS na siku ya tatu itakuwa ni kwa ajlia ya ufungaji rasmi na kilele cha maadhimisho hayo.
Kutokana na maadhimisho hayo, wageni rasmi wanatarajiwa kuwa viongozi wakuu wan chi hii ambao watatumia maadhimisho hayo kufikisha ujumbe wenye kuleta mwasho na ustawi wa SACCOS nchini Tanzania.

Aidha, wana saccos watatumia fursa hiyo kufikisha ujumbe wao kwa viongozi  hao ili kuzipatia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazowakabili hadi sasa.
Kwa kuzingatia hizi ni sherehe kubwa kwa Wana saccos kote Duniani, kwa vyovyote gharama za kufanikisha sherehe hizi, hivyo kamati ya fedha na Mipango imeamua kuzigawanya SACCOS katika makundi kulingana na jinsi zilivyo, ambapo lipo kundi la SACCOS zinazoombwa kutoa mchango wa Tshs.200000/= ili kufanikisha shughuli hiyo.
Mchango huo utakuwa na utaratibu maalumu katika malipo, ambapo kamati ya maandalizi kupitia “account” kama ifuatavyo:,

SCCULT-ICUD ACCOUNT
CRDB BANK, LUMUMBA BRANCH
ACCOUNT NO. 0150270503200
Baada ya kufanyaa malipo hayo, tafadhali wasiliana na yeyote kati ya walioorodheshwa hapa chini kwa ajili ya kupatiwa takabadhi husika
Mtunza Hazina wa kamati ya John Fidelis Komba kwa mob: 0655414992
Mtunza Hazina msaidizi Somoe Ismail Nguhwe kwa mob: 0754527249
Mtunza kumbukumbu za ICUD kifedha Ahmad Mushumbusi kwa mob: 0715917993


Mwenyekiti wa kamati ya fedha Jostus Masengo kwa mob: 0713711249
Aidha mnakaribishwa kwenye maonesho na kongamano kama ilivyooneshwa hapo juu ili kwa pamoja tufanye tathimini ya mafanikio na changamoto zinazozikabili SACCOS za Tanzania.
Iwapo SACCOS moja wap inakusudia kushiriki kwenye maonesho hayo, tafadhali tujulishwe mapema kwa kutumia anuani ya barua , simu au email iliyoko hapo juu.
Kwa watakao thibitisha kushiriki maonesho wakati wa maadhimisho hayo kamati husika itatumia vigezo vya mashindano ili kuwaandaa kuingia kwenye mashindano ya SACCOS Bora kwa mwaka 2016 kupitia maadhimisho haya.

Mbali na kamati kulipia gharama zote za banda la maonesho, waoneshaji wawili wa SACCOS husika watalipwa nauli kwa siku zote tatu watakazo kuwa wamehudhuria na kiwango cha nauli kitakuwa Tsh.10000/= kwa kila mmoja, na kamati ya maadhimisho imeandaa zawadi nono kwa washindi wa mashindano ya SACCOS bora 2016, hivyo msikose fursa hii.
Kamati ya maandalizi inawashukuru huku ikitarajia kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau wake wa SACCOS, ikiwa ni pamoja na kupokea mchango wenu kabla ya tarehe 15 septemba.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.