Na Issa Ramadhani
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watu sita wameuwawa nchini Kenya katika shambulizi linalohisiwa kufanywa na kundi la al-Shabaab katika eneo la makazi la Bulla katika mji wa Mandera.
Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo wakati wapangaji wa eneo hilo wakiwa wamelala, ambapo polisi walifanikiwa kuwaokoa watu 25.
Kufuatiwa na tukio hilo la kigaidi, Polisi wamesema washambualiaji hao waliwafyatulia hovyo risasi wapangaji wa makazi hayo baada ya kuvunja na kuingia kwenye makazi hayo.
Kundi hilo la wavamizi lilitumia bomu la mkono kuvunja na kuingia katika makazi hayo na kisha kuwafyatulia risasi watu waliolala na baadaye kutoroka kunako sehemu isiyojulikana.
Shambulio hilo sio la kwanza kutokea kwa kikundi hicho cha ugaidi cha Al-Shabaab, kwani imekua ndio desturi yao kukamata watu na kulipua maeneo mbali mbali na kupelekea idadi kubwa ya vifo vya watu wasio na hatia
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment