Halloween party ideas 2015
Image





Na Yusuph Mwamba.
KLABU  ya soka ya Manchester United, ipo mbioni kuvunja bank kwa ajili ya kunasa saini ya mwanandinga wa kimataifa wa Ufaransa Poul Pogba anayekipiga kunako klabu ya Juventus ya Italia.


Pogba ,mwenye umri wa miaka 23, ambye alikipiga kunako klabu ya Manchester United mwaka 2012, amabpo timu hiyo ilikuwa chini ya aliyekuwa Meneja wa zamani wa klabu hiyo, Sir Alex Furguson.
 Licha ya Real Mdrid kujitoa katiaka mchakato wa kuwania saini ya Nyota huyo, lakini Man United imeonekana kuweka nguvu katika kuwania saini ya mwanandinga huyo huku ikiwa tayari kuvunja rekodi ya Dunia kwa kumpa dili la  £87m sawa na 104m Euros


Mpaka sasa mambo yanaonekana kwenda vizuri huku Uongozi wa klabu ya Manchester United ukiwa umekutana na uongozi wa klabu ya Juventus pamoja na wakala wa mwanandinga huyo ajulikanya kama Mino Raiola, Japo kuwa Juventus wakionesha nia ya kutaka kumuongezea mkataba mwanandinga huyo ili kuendeklea kuwatumikia vibibi kizee wa Turini.
Raiola ambaye ni wakala wa mwanandinga huyo yupo mapumzikoni Empolio wakati mwanandinga huyo akiendelea na likizo yake nchini Ufaransa na anatarajia kurejea kunako klabu yake ya Juventus ya Turini ifikapo Augusti 6, 2016.

Chanzo chetu cha Sky Sport kimeripoti kuwa, Pogba, ameshakubaliana na dili la mshahara kunako klabu ya Manchester United huku malipo yake yakiwa ni pauni milioni 300 kwa wiki wakati kwa mwaka atakuwa amejikusanyia kitita cha fedha chenye thamani  £10.92m sawa na 13m Euros kwa mwaka kama ada ya mshahara wake kwa mwaka mzima ambapo hayo waliafikiana wiki iliyopita pindi alipokwenda  and his path to Old Trafford baada ya Real Madrid kujitoa katika kinyang'anyiro cha kuwania saini ya mwanandinga huyo.

Pogba, aliondoka kunako   Old Trafford akiwa mchezaji huru mwaka 2012 lakini anatarajia kurudi kama mfalme na kuvunja rekodi ya Dunia katika dili la uhamisho ambapo dili hilo linaweza kukamishwa mwanzoni mwa mwezi Augusti kama makubaliano yatakwenda vizuri.
Meneja mpya wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, amesema kuwa katika mapendekezo ya usajili alishatoa vipaumbele kwa nyota wanne ambao wataweza kuungana naye katika mapambano ya ushindi huku akiwataja baadhi ya nyota hao wakiwemo Henrikh, Zlatan Ibrahimovic na mlinzi wa kati Eric Bailly huku akisubiria saini ya Poul Pogba. Mkhitaryan,capture marked their third acquisition following the arrivals of Zlatan Ibrahimovic and centre-back Eric Bailly.

Pogba, ni miongoni mwa nyota walioweza kufanikiwa kuifikisha timu ya Taifa ya Ufaransa fainali ya michuano ya kombe la Euro 2016 japo walishindwa kutwaa ndoo hiyo baada ya kupokea kichapo kutoka kwakwa timu ya Taifa ya Ureno kwa bao 1-0 nakuifanya Ureno kuibuka kinara wa michuano hiyo aliyokuwa akicheza pasipo na mafanikio kwa muda mrefu sana.
Mpaka sasa Pogba , amefanikiwa kusherekea ubingwa wa Italia akiwa na klabu yake ya Juventus mara nne katika ligi kuu ijulikanayo kama Serie A huku akifanikiwa kuiwezesha klabu ya Juventus kuchukua Copa Italia mara mbili.



JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install
App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.