Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

ZIKIWA zimepta takeibani siku 85 ,tangu kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni 21 April 2016 Ally Salum Hapi, ameendelea kutekeleza kwa vitendo majukumu aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli.


Licha ya kusimamia suala la watumishi hewa katika wilaya yake ambao walikuwa 34 na kufikia 101, huku akisimamia vyema na Kulimaliza suala la upatikanaji wa madawati katika wilaya yake ambapo imekuwa changamoto kubwa tangu kutangazwa kwa Elimu bure.



Mkuu wa Wilaya Ally Salum Hapi ,ameelendelea na kasi hiyo ya HAPA KAZI TU, ambapo siku ya leo ametembelea maeneo ya Tandale Hospitali, Uwanja wa Fisi na Soko la Tandale kwa ajili ya kusikiliza kero za wakazi wa maeneo hayo.

 

Akizungumza  na wakazi wa Tandale, Mkuu wa Wilaya, amewataka kuzingatia suala la usafi na kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kuwekea uchafu katika maeneo yao huku akiwasisitiza wale wenye sehemu za kuegeshea magari kuyaweka katika mazingira ambayo hayataleta athari za kimazingira.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline







Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.