Ndege ya
shirika la ndege la Misri la EgyptAir iliyokua ikitokea Jumatano usiku katika uwanja wa mji wa Paris ikielekea Cairo, nchini Msri imetoweka kutoka kwenye mitambo ya rada, ikiwa na abiria 56 na wafanyakazi 10, shirika la ndege la Misri limetangaza mapema Alhamisi hii asubuhi.
Ndege hii imetoweka ghafla kutoka kwenye mitambo ya rada wakati
ambapo ilikua ikipaa angani katika eneo la bahari ya Mediterranean.
Ndege hii ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir iliyokua ikitokea
katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris ikielekea Cairo,
nchini Msri, imetoweka Alhamisi hii asubuhi na mapema, ikiwa naabiria
56 na wafanyakazi 10.
Ngege hii yenye chapa MS804 ilikua ikipaa katika eneo la bahari ya Mediterranean katika anga baa ya kuingia kilomita 16 katika anga ya Misri.
Shirika la ndege la EgyptAir limeonya mamlaka husika na kusema kuwa timu za waokoaji zimeanza shughuli ya kutafuta ndege hiyo, na kubainisha kuwa "ndege imetoweka kwa rada" baada ya kuingia katika anga ya Misri na kusafiri kilomita 16.
Abiria waliokuwemo ndani ya ndege A320
Awali, shirika la ndege la EgyptAir ilitangaza kuwa kulikuwa na abiria 59 na wafanyakazi 10. Kwenye akaunti yake Twitter, EgyptAir hatimaye imesahihisha takwimu zake, na kusema kwamba kulikuwa na abiria 56, ikiwa ni pamoja na watoto 3 - na wawili wachanga. Wafanyakazi 7 walikuemo ndani ya ndege hiyo pamoja na maafisa 3 wa usalama. Kwa jumla, watu 66 walikuemo ndani ya ndege hiyo.
Kwa mujibu wa EgyptAir, Wafaransa 15, Wamisri 30 walikua ndani ya ndege hiyo, pamoja na raia 1 wa Columbia, raia 1 wa Ubelgiji, raia 2 wa Iraq, raia 1 wa Kuwait, abiria mmoja wa Saudi Arabia, rara 1 wa Sudan, raia 1 wa Chad, raia 1 wa Ureno, raia 1 wa Algeria na raia 1 wa Canada.
source-rfikiswahili

Post a Comment