Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani


MSHINDI mara mbili wa mashindano ya Australian Open ,Victoria Azarenka , amefichua kuwa anamimba.

Raia huyo wa Belarus mwenye umri wa miaka 26, amesema anapanga kurejea katika uchezaji baada ya kujifungua mwishoni mwa mwaka huu.





Azarenka na mpenzi wake, waligundua kwamba alikuwa mjamzito alipokuwa anauguza jeraha lake la  goti.

"Tuna furaha sana na najihisi kubarikiwa kuwa Mungu akipenda nitaanza safari hii ya kusisimua,” amesema Azarenka, ambaye ameorodheshwa na kukamata nafasi ya sita  kwa ubora duniani.




"Nimetiwa moyo sana na wanamichezo wengine wa kike ambao huweza kurejea kushindana baada ya kujifungua na ninapanga kufanya hivyo hivyo.”
Azarenka ,alishinda Australian Open mwaka 2012 na 2013, miaka ambayo pia alifika fainali US Open lakini akashindwa.


Hajacheza tangu aondoke uwanjani raundi ya kwanza mechi ya French Open dhidi ya Mwitaliano Karin Knapp mwezi Me

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline




Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.