HIVI Karibuni, itakuwa hauhitaji cheti hicho madamu wewe ni mwafrika !
Kisa na maana ,,,, Bara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!
Madhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho, ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.
Viongozi wa kiafrika wamezindua cheti hicho maalum mjini Kigali Rwanda, katika kongamano la viongozi wa Afrika.
Wakwanza kupewa cheti hicho watakuwa ni viongozi wenye hadhi ya kupewa vyeti vya kidiplomasia.
Viongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyejiwa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby
Marais wote waliohudhuria kongamano hilo watapewa cheti hicho cha AU kabla ya kukamilika kwa mkutano huo.
Mawaziri wa maswala ya kigeni na viongozi wakuu katika umoja wa Afrika pia wanatarajiwa kufaidi cheti hicho cha kusafiria.Umoja wa Afrika unatarajia kuwa mataifa ya kiafrika yataanza kutoa vyeti hivyo vipya vya usafiri kufikia mwaka wa 2018.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment