KLABU ya soka ya Chelsea ipo mbioni kumwania nyota wa Inter- Milan, Joao Mario, wakati huo huo klabu ya Borussian Dortmund ipo mbioni kunasa saini ya mwanandinaga anayekipiga kunako klabu ya Newcastle United, Moussa Sissoko.
Schalk 04 yakuabliana na klabu ya Manchester City juu ya kumnyakua mshambuliaji wao hatari Leroy Sane, kwa ajili ya kutumikia klabu hiyo msimu ujao, huku klabu ya soka ya Einracht Frankfurt imeonesha nia ya kumuhitaji kinda wa Manchester United, Guillermo Varela kwa mkopo
Newcastle mbioni kunasa saini ya aliyekuwa mwanandinga wa zamani wa klabu ya soka ya Liverpool, Peter Crouch kutoka Stock City, huku Hull City ikionekana kutaka kumarisha safu ya ulinzi kwa upande wa golikipa baada ya kuwa na nia ya kuhitaji saini ya golikipa wa Cardff , David Marshall
Timu ya Taifa ya Ukraine, imesthibitisha miapango ya kumkabidhi timu aliyekuwa kocha msaidizi wa ntimu hiyo, Andrly Shevchenko kuwa kocha mkuu, wakati huo huo Uongozi wa Uingereza unaamini kuwa huenda ndoto za Sam Allardy kuongoza Timu ya Taifa ya Uingereza kuyeyuka, baada ya chama cha soka cha mpira wa miguu Uingereza FA , kupokea taarifa juu ya kocha wa Ujerumani , Jurgen Klinsmann
Klabu ya soka ya FC Basel, imesema ipo mbioni kunasa saini ya nyota wa kimataifa wa
Colombia, Eder Alvarez Balanta kwa kandarasi ya miaka minne, Balanta mwenye umri wa miaka 23, amekuwa mchezaji wakwanza kuwaniwa na kabu hiyo akitokea Ligi ya Argentina kunako klabu ya River Plate.
Dortmund wapo mbioni kunasa saini ya mwanandinga wa kalbu ya soka ya Wolfsburg na aliyekuwa nyota wa zamani wa klabu ya soka ya Chelsea.Andre Shurrle mwenye umri wa miaka 25.
Meneja mpaya wa klabu ya soka ya Manchester City, Pep Guardiola, amesema atatumia kiasi cha Euro milioni 100 kwa ajili ya kuanasa saini ya wanandinga atako wahitaji kama John Stones na ,Leroy Sane, kwa jumla ya pauni milioni 35, lakini mpaka sasa klabu hiyo imefanikiwa kuwasajili nyota wawili akiwemo Gundogan na Nallito
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment