WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Kassim Majaliwa ameagiza kila Halmashauri kuhakikisha wanapima maeneo, kutoa hati na kutenga maeneo ya uwekezaji ili kuondoa usumbufu pindi wawekezaji wanapokuja kuwekeza.
Akizungumza na waandishi wa habari Kibaha, Majaliwa , amesema kuwa wapo baadhi ya viongozi wanaendekeza urasimu na kusababisha wawekezaji kutovumilia hivyo kwenda kuwekeza nje ya Tanzania.
Majaliwa , aliyazungumza hayo pindi alipotembelea kiwanda cha Nondo jana kinachomilikiwa na kikundi cha Kilua, Kijiji cha Disunyara , Mlandizi , Wilayani Kibaha.
"Serikili yetu imepanga mikakati ya kuondoa urasimu wa kupata hati , Halimashauri zote Nchini nawaagiza sasa pimeni maeneo yote na mtoe hati tufanye hinyo ili kuwarahisishia Wananchi na wawekezaji".Alisema Mjaliwa
Aidha, alimtaka Mkurugenzi wa Shirika la Reli, kuhakikisha anaendelea kusimamia uboreshaji wa miundombinu ya Reli ifike kwenye maeneo ya Viwanda na kurahisisha usafirishaji wa malighafi zinazozlishwa.
Mkurugenzi wa Kilua Group,Mohamed Kilua, ambaye ameshirikiana n rafiki zake raia wa China kujenga kiwanda hicho amesema kuwa kikikamilika katika awamu ya kwanza kitaajiri Vijana 100 hadi 300 na katika awamu ya tatu kitaajiri Vijana 300 hadi 800 watakuwa wamepata ajira
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment