Na Yusuph Mwamba
KLABU ya soka ya Simba SC chini ya Kocha mpya wa sasa ya kocha ,Joseph Omog, kimepanga kwenda kuweka kambi yake Mkoani Morogoro kam moja ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara VPL 2016/2017 kikosi cha Simba sasa kitaingia kambini Mjini Morogoro kujiimarisha zaidi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Omog ambaye amemwaga wino wiki iliyopita na kukubali kukinoa kikosi cha Msimbazi, tayari ameshaweka wazi mipango yake juu ya kambi kwa ajili ya mawindo ya ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao huku akianza mazoezi na baadhi ya nyota wake wapya kwenye uwanja wa Bandari uliopo kurasini. |
Joseph Omong Kocha wa Simba SC |
Omog ,amekuwa akitumia muda mwingi kuwapa mazoezi ya kukimbia uwanja kwa saa tatu pamoja na mazoezi ya viungo, lengo likiwa ni kuwatengenezea wanandinga wake stamina na pumzi ili wamudu waweze kudumu ndani ya dakika 90 za mchezo wawapo uwanjani..
“Nimewapa mazoezi ya kuongeza stamina, nguvu na pumzi ili wachezaji wangu wamudu kucheza mpira kwakuwa wachezaji wengi wanakuwa wazito kwa mazoezi haya naimani nitwaweka fitness na kudumu mchezo ndani ya dakika zote wawapo Dimbani".Alisema Omong
Pia Kocha huyo aliongeza kwa kusema wachezaji wengi haswa wa kitanzania wanauvivu wa kufanya mazoezi haswa mazoezi ya kutafuta pumzi kwao yamekuwa kama ugonjwa sugu ila kwa kuwa hilo ni tatizo nimeona nilipatie ufumbuzi kwa wachezaji wangu
“Nimefikia hatua hii baada ya kuwaona wachezaji wanachoka mapema baada ya kuwapa mazoezi ya kukimbia mbio ndefu na fupi, ninataka timu imudu kucheza dakika zaidi ya 90 katika mechi,” Alisema Omog.
Kocha huyo mara baada ya kusaini na klabu hiyo ya Simba , Omong ameapa msimu ujao Simba inapanda ndege kushiriki michuano ya kimataifa kwani atahakikisha Wekundu hao wa Msimbazi wanamaliza ukame wa mataji.
Licha ya kuanza na mazoezi hayo pia kocha huyo amesema kuwa amekuja na mifumo mingi mpaka sasa hajajua atumie mfumo upi ambao utaendana na kikosi chake kitu ambacho mpaka sasa amekiri kutowafahami vizuri wanandinga wake kwamba atakapokaa nao angalau kwa wiki mbili zaidi atajua ni mfumo upi sahihi wa kwenda nao kutokana na aina ya wachezaji wake alionao kunako kikosi hicho.
Kikosi cha Simba ,kinatarajia kujichimbia Mkoani Morogoro kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuvuka maji na kuelekea Zanzibar ambapo nako wataweka kambi ya muda wa wiki mbili huku ikiwa moja ya maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania bara inayotarajiwa kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu.
Hata hivyo, kabla ya mchakamchaka wa ligi timu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki na Gor Mahia kwenye tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment