NAIBU waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Angelina Mabula, amekitaka Chama cha Waendelezaji Miliki hapa nchini kujenga ufahamu kwa jamii kuhusu sekta hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, jana Jijini Dar es salaam,wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau endelezaji miliki, Mabula amesema mbali ya ufahamu wa mtu mmoja mmoja , bado kama Taifa hawana ualedi juu ya sekta hiyo ikiwemo taarifa sahihi .
Aidha Waziri Mabula alisema kuwa , kuanzishwa kwa chama hicho kuwe chachu ya kusimamiana wenyewe , kwa baadhi ya waendelezaji miliki wamekuwa wakivunja sheria ikiwemo kujenga katika viwanja ambacyo hawavumiliki kisheria na maeneo ya wazi.
Licha ya Mabula kuzungumza hayo, naye Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi , Nehemiah mchechu, amesema lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni kutetea masilahi ya waendelezaji miliki wote nchini.
Mchechu ,ameyazungumza hayo mbele ya waandishi wa habari huku akisema , chama hicho kitakuwa kikisimamia maadili ya waendelezaji miliki nna kuwashawishi wanachama wake kuzingatia sheria na kushindana kibiashara ili kujikwamua kiuchumi,
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment