Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani

WATANZANIA wanatakiwa kuzingatia suala  la  ulaji wa vyakula na kujali afya, kwa kula  vyakula vya kujenga mwili na akili pia, utamaduni  huu  utasaidia sana kwa viazazi.

Kwa mujibu wa utafiti wa wataalamu mbalimbali na wanasayansi wamekubali  kuwa ulaji wa vyakula vifuatavyo ni muhimu sana  kwa binadaamu .

Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:


1.MAFUTA YA SAMAKI





Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu. Ulaji wa samaki hasa wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.


2.PILIPILI KALI

Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika ya kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.


3.MBEGU ZA MABOGA






Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa ni vizuri.


4.NYANYA





Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya hasa za kuiva utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.


5. BROKOLI




Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.


6.KARANGA



Aina zote za karanga mbichina kavu zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.


7.MAYAI





Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

Hivyo ni muhimu sana kujali afya yako  , ili  kuepukana ana magonjwa, yasikuwa na tija kwa kuimalisha  kinga  ya mwili kwa  kuwa na ulaji mzuri hasa  mli kamili,kwani  bora kinga kuliko tiba wanadamu tunapaswa kujali afya zetu kwanza, maaana afya  iamra ndo msingi wa kufanya  kazi na kuwa na akili ya kufanya kazi na mambo mbalimbali





JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline




Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.