RAIS wa Taifa la Ureno, Marcelo Rebelo De Sousa ,amekuwa na majigambo mengi pindi anapohojiwa na vyombo vya habari ikiwa ni baada ya timu yake ya Taifa ya Ureno ,kufanikiwa kutwaa kombe la Euro 2016 lililomalizika hivi punde ambapo Ureno ilifanikiwa kuinyuka timu ya Taifa ya Ufaransa wenyeji wa mashindano kwa bao 1-0 .
Rais De Sousa ,amesema mapaka sasa anatafakari zawadi ya kuwapa mabapo aliwaita Mashujaa wa Euro 2016 baada ya ahadi ya kwanza kuikamilisha katika mapokezi ya timu hiyo juzi yaliyopokelewa kwa shangwe kubwa na mamia ya mashabiki waliojitokeza kuwalaki mashujaa hao.
"Ushindi huo walioupata mashujaa hao nia faida kubwa kwa Taifa pamoja na kila mmoja akishangilia mafanikio hayo ambayo ni makubwa sana zaidi ya kuwahi kuyapata katka historia ya siku za karibuni".Alisema De Sousa
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment