Na Yusuph Mwamba
KUMEKUWA na kawaida sana kwa jamii ya sasa kusikia kuwa msichana kaolewa na mvulana aliyemzidi aliyemzidi umri hiku Mvulana naye akio Msichana aliyemzidi umri, jambo ambalo kwa sasa limekuwa kama utamaduni wetu kwa kile kinachodaiwa kulelewa.
Lakini hiyo haitoshi mtazamo hasi ndio umekuwa ukitumika zaidi katika ndoa hizi huku kila mmoja wao akivutia kwake kwa sababu maalumu anazozitoa bila kungalia madhara ya kufanya jambo hilo kwa upana yote imetokana na kukosa Elimu ya Uzazi pamoja na maswala ya ndoa.
Zamani Babu na Bibi zetu walikuwa wakitumia kanuni hizi za umri lakini maadili yalikuwa mapana mno tofauti na dhama za sasa mambo yanaonekana kubadilika mno kiasi kwamba mkwe na mkwewe wakiketi pamoja na kupiga stori wakati zoezi la Ndoa kabla halijafanyika huku watoto wa Mjini wakiuuita Utandawazi.
Inawezekana kabisa kwa Msichana mdogo kuwa na mahusiano ya Kimapenzi na Mwanaume mwenye umri mkubwa.
Hata hivyo,uzoefu umeonyesha kwamba Mahusiano kama haya mara nyingi yanakuwa magumu kutokana na sababu zifuatazo.
SUALA LA UPEVU WA AKILI NA UWIANO WA JINSI YA KUFURAHIA MAISHA.
Kwa mfano, Vijana ambao hawajapishana sana umri ( Miaka ishirini na zaidi) wanaweza kuongea, kujadiliana na kuelimishana kuhusu mambo yao, Lakini inapokuwa umri umepishana sana, mvuto wao wa maisha unakuwa tofauti vile vile.
Kwa kuongeza, mzunguko wao wa watu wa rika utakuwa wa umri tofauti na watakuwa na mambo machache sana ambayo yatawafurahisha wote wawili kwa pamoja. Mara nyingi , hili hili linaweza kuleta mtafaruku kati ya Msichana na Mume wake na kusababisha kuwa na Uhusiano wa juu juu.
KUNA SHAKA KIDOGO KUHUSU KULEA WATOTO
Kumlea mtoto mapaka afikie umri mkubwa wa kuweza kujitegemea na kufanya maamuzi yake mwenyewe, kunahitaji nguvu nyingi sana.
Sasa iwapo mume naye amezeeka na anahitaji kutunzwa itamuwia vigumu sana Mwanamke kutekeleza majukumu yote kwa ufanisi , ili kuhakikisha maendeleo mazuri ya familia.
Kwa kuongeza, Mwanaume mzee anaweza kupunua nguvu ya hamu ya kutaka kujamiana wakati wa Msichana hamu yake ipo juu. Hili linaweza kuleta ugomvi mkubwa kati yao.
Unapofikiria Mahusiano na Mwanaume mwenye umri unaozidi umri wako sana, fikiri hoja zilizoandikwa hapo juu na angalia hali yako.Maranyingi ni rahisi kudumisha mahusiano, ukiolewa na mtu ambaye mnalingana umri.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment