Halloween party ideas 2015
Image

Na Mwandishi wetu


Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionShule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu.

Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu.
Shule ya Dargh-E-Ala Hazrat inayodhibiti madrassa 15,000 za Kiislamu ilitangaza hilo kufuatia agizo la mahakama lililopiga marufuku talaka za moja kwa moja.
Wasomi wa Kiislamu wamedai kwamba talaka za moja kwa moja haziambatani na sheria ya kiislamu.
Kiongozi mmoja wa dini kutoka shule hiyo amesema kuwa wataanzisha kifungu kitakachoangazia maswala ya talaka.
Mtaala wa shule hiyo ambao unaangazia Koran na sheria za kiislamu unazungumzia kuhusu talaka lakini sio kwa maelezo ya kina.
''Tulifanya mkutano wa viongozi wa dini pamoja na wale wa Madrassa baada ya agaizo la mahakama kuu na tumewaelezea jamii kupitia wanafunzi na katika ibada za siku ya Ijumaa kuhusu njia bora za kutoa talaka'', Maulana Shanbudin Racvi kiongozi mkuu wa dini aliambia BBC Hindi.
Aliongezea kuwa hatua hiyo itaelezea vyema kwamba talaka ya moja kwa moja zinazoetekelezwa nchini India haziambatani na sheria za Kiislamu.
Haijulikani ni umri upi wanafunzi hao wote wakiwa wavulana wenye kati ya miaka mitano hadi 16 watafunza kuhusu talaka.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.